
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
Ameyasema hayo leo bungeni, Lukuvi amesema lengo ni kuhakikisha hakuna ubabaishaji kwenye sekta ya ardhi hasa katika uwekezaji.
Amesisitiza hayo wakati Mhe. Lukuvi baada ya kukukutana na kutoa hati za malipo kwa makampuni 14 ya uwekezaji wa viwanda mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kutaka kuondoa vikwazo kwa wawekezaji ambao wengine walikimbilia nchi za nje kuwekeza baada ya kukwama nchini.
Mbali na hapo Mhe. Lukuvi ameagiza utoaji wa vibali vya ardhi ufanyike ndani ya wiki moja mara tu serikali inapojiridhisha na maeneo husika wanayoombwa ili kuepusha migogoro na wananchi wa maeneo husika nakutoa onyo kali kwa wawekezaji waliobadilisha matumizi kuwasaka nakuchukuliwa hatua za kisheria kwa haraka.
Nao wakuu wa mikoa minne ambao wamewapokea wawekezaji hao katika mikoa yao wamesema watatoa ushirikiano mkubwa kwa wawekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi kuwekeza nchini.