Walioiba zaidi ya Bil 1 za NMB wakamatwa

Jumatatu , 6th Jul , 2020

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi jijini Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametoa onyo kwa wanaojiandaa kufanya maandamano siku ya tarehe saba kwa lengo la Kudai Tume huru ya Uchaguzi.

Kamanda Mambosasa

Mambosasa ameyasema leo Julai 6, 2020 mbele ya waandishi wa habari, ambapo amesisitiza kuwa wahalifu wote na wasiofuata sheria za nchi wataendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha Kamanda Mambosasa, amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum limewakamata wahalifu 32 ambao walihusika na wizi wa mabilioni ya fedha kwenye Benki ya NMB. 

Amesema wahalifu hao walikuwa wakihusika na wizi wakati wa usindikizaji wa fedha kupeleka katika matawi mbalimbali ya benki  hiyo.

Pia Mambosasa ametaja baadhi ya vifaa ambavyo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limevikamata baada ya kuwa vimeibiwa ni pamoja na Pesa na Vifaa vya ndani.