
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo mkoani Tanga, wilayani Pangani wakati alipotembelea moja ya shule ya kidato cha tano na sita, ambapo alieleza kusikitishwa na shule hiyo kukosa wanafunzi wa kidato ha sita kwa sababu zisizo na msingi.
Waziri Jafo amesema kuwa, "yaani hamkuweza kukamilisha nondo kwenye madirisha, na vitanda kumi na suala la maji, sasa niwaulize yaani vitu hivyo ndiyo zimesababisha wanafunzi kutokuja hapa kusoma?"
"Unajua tukiwa na watu waliokulia mboga nane nchi hii haiendi, sisi wengine ni watoto wa kimaskini tumekulia nchi ya kimaskini, nimetembelea kule Uyui mtoto anatembea Kilometa 15, lakini amefaulu kwa Div 3, ila anakosa shule kwa sababu hazipo ila ajabu hapa zipo, wakati mwingine wataalamu wa Serikali nyinyi ni matatizo" amesema Jafo.
Aidha Waziri Jafo amesema suala hilo kuna baadhi ya wataalam walizembea na atahakikisha baadhi yao watachukuliwa hatua.