Jumanne , 12th Oct , 2021

Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, amesema kuwa upelelezi wa watu waliohusika na tukio la kupigwa risasi kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, unaendelea na wahusika wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene

Waziri Simbachawene ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kupitia ITV, na kusisitiza kwamba Jeshi la polisi linazo kesi nyingi za aina hiyo hivyo haliwezi kufanya upelelezi maalum kwa ajili ya mtu mmoja peke yake.

"Tuna kesi nyingi sana, hiyo kesi unayoisema ambayo sitaki hata kuitaja ni miongoni mwa kesi tunazozipeleleza, hatuwezi kuwa na specialization kwa ajili ya kesi ya mtu mmoja tunapeleleza kwa mujibu wa sheria na tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria, hivyo upelelezi na uchunguzi unaendelea pale ambapo tutakuja kuwapata wahusika tutawafikisha mahakamani," amesema Waziri Smbachawene.