
Wananchi waliopanda Mlima Kilimanjaro
Akieleza kuwa kitendo hicho ni cha kishujaa na uzalendo mkubwa kwa nchi.
Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa kuendelea kuwahamasisha wananchi na wadau mbalimbali kupanda Mlima Kilimanjaro ili waweze kufurahia mandhari na kupata elimu ya uhifahdi wa maliasili pamoja na kujifunza zaidi kuhusu Uhuru na historia ya Taifa la Tanzania.
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya maboresho makubwa kwenye maeneo ya Hifadhi za Taifa ukiwemo Mlima Kilimanjaro ili kuweka mazingira rafiki kwa wageni wanaotembelea vivutio hivyo akitoa wito kwa wananchi na Wadau mbalimbali kufaidika na maboresho hayo.
Ikumbukwe kuwa tarehe 5 Desemba ,2022, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana alikabidhi Bendera ya Taifa kwa wapandamlima zaidi ya 200 waliokuwa wakielekea kilele cha Mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru.