
Eneo la 14 Riverside Jijini Nairobi
Tukio hilo lililotokea jana, Januari 15, lilianza saa 3:30 asubuhi, ambapo makundi ya wafanyakazi wapatao 150 walikuwa wakisindikizwa kwaajili ya kupata hifadhi na wengine wengi wakisalia ndani wakipewa huduma ya kwanza kutokana na majeraha.
Ofisa mmoja wa serikali ya Marekani aliuambia mtandao wa Reuters kuwa miongoni mwa watu hao waliouawa, mmoja ni raia wa Marekani.
"Tunathibitisha kwamba raia mmoja wa Marekani ameuawa katika shambulio hili", amesema Ofisa huyo bila kueleza zaidi taarifa zaidi juu ya tukio hilo.
Ikumbukwe kuwa nchi ya Kenya imekuwa ikivamiwa ikilengwa na kundi la Al Shabaab tangu mwaka 2013, ambapo ilivamia jengo la kibiashara la Westgate Jijini Nairobi na kuua watu 67.
Pia shambulio lingine lililotekelezwa mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa, liliua wanafunzi 150 ambapo kikundi hicho kilijigamba kuwa ni kulipiza kisasi kwa kile walichodai nchi hiyo kuingilia mgogoro wa Somalia, baada ya kupeleka wanajeshi wake wa kulinda amani nchini humo.