
Kinyonga
Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro, imesema kuwa Wizara hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vilifanya uchunguzi kuhusu tukio hilo la usafirishaji wa wanyamapori hao.
"Uchunguzi huo umeonesha kwamba siyo tu vinyonga 74 kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari lakini pia kulikuwa na nyoka sita na uchunguzi umewatia hatiani Watanzania wanne na wamekiri kuwauzia wazungu wawili," ameelezea Dk. Ndumbaro.
Katika hatua nyingine Dk. Ndumbaro, amewataka Watanzania kuwa wazalendo kwa kulinda wanyamapori ili kutoathiri uchumi wa sekta ya utalii kutokana na serikali kusitisha usafirishaji wa wanyamapori hai tangu Mei 2016.