Ijumaa , 7th Aug , 2015

Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wanaosadikiwa kuwa ni wanachama wa chama cha Mapinduzi, jana wameivamia ofisi ya chama hicho ya wilaya ya Sumbawanga mjini,

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa Ndugu Hiporatus Matete akizungumza kwenye ufunguzi wa semina.

Wananchi hao wametoa samani zote zilizoko kwenye ofisi ya mwenyekiti wa wilaya hiyo na kuzitupa nje, kwa kumtuhumu kuwa ameongoza vikao vilivyokata jina la mbunge anayemaliza muhula wake Aeshi Hilal aliyeshinda kwenye kura za maoni.

Wakiongea kwa jazba mbele ya ofisi hizo za CCM, Wilaya ya Sumbawanga kwenye barabara ya sokoine mjini Sumbawanga, wamesema hata siku moja hawawezi kuvumilia vitendo vinavyofanywa na Mwenyekiti wa CCM, wa wilaya hiyo Bw, Selemani Kilindu kwa chuki binafsi.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM, wilaya ya Sumbawanga mjini Bw, Enos Budodi, amepata wakati mgumu mno akijitahidi kuwatuliza bila ya mafanikio kuwa haki lazima itendeke.

Katika hali inayoashiria kuwa mambo si shwari hata kwenye jimbo la Kwela wilaya ya Sumbawanga vijijini, ni jinsi baadhi ya wagombea wa jimbo hilo walivyolaani kitendo cha Katibu wa CCM, wa wilaya hiyo Bw, Albert Stima, kutangaza matokeo kinyume cha makubaliano ya awali, kwamba hadi matokeo ya kata mbili zilizosalia yapatikane, na kusema kuwa wanakusudia kuwasilisha malalamiko yao kwenye vikao vya juu