Ijumaa , 17th Apr , 2015

Zaidi ya wanafunzi 230 wa shule ya msingi linda katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, wamekosa madarasa ya kusomea na kulazimika kusomea chini ya miti ya mikorosho kutokana na kuezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali tangu julai mwaka jana

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw, Essau Ndunguru amesema kwa miezi 10 wanafunzi wamekuwa wakisomea chini ya miti ya mikorosho na pindi mvua zinaponyesha hulazimika kusitisha masomo kwa muda.

Amesema uwezo mdogo wa kifedha wa wazazi ambao asilimia kubwa wanategemea kipato chao kutokana na uvuvi wa samaki wameishia kufyatua tofari pekee na kushindwa kugharamia vifaa vya kiwandani ikiwemo mabati

Nao wakazi wa Kijiji hicho wameimba Serikali kusikiliza kilio chao ili wawezae kujikomboa kutoka katika janga hilo aidha waweze kurekebisha mambo mengine ya kielimu ikiwemo kuwaongezea walimu ili watoto wao waweze kupata elimu bora.

Pamoja na kamanda wa vijana (UVCCM) wilaya ya Nyasa, Bw. Cassian Njowoka aliyesimikwa ukamanda huo siku za hivi karibuni kutembelea shule hiyo na kuchangia bati 90 kuunga mkono bati 60 alizotoa marehemu Kepten John Komba kabla ya kifo chake Februali 28 mwaka huu, wananchi nao wanaiomba serikali na wadau mbalimbali kuwaunga mkono ili kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo.