Jumatano , 26th Oct , 2022

Watawala wa kijeshi nchini Burkina Faso wameanzisha harakati za kuajiri maelfu ya raia wanaojitolea kusaidia kupambana na wapiganaji wenye itikadi kali za Kiislamu.

 

Kamanda wa kikosi hicho kinachoitwa Volunteers for the Defence of the Fatherland, alisema lengo ni kuandikisha wanachama wapya 35,000.

Wagombea watapata mafunzo ya kijeshi ya wiki mbili kabla ya kushiriki katika operesheni kote nchini humo, ambayo imekuwa ikipambana na uasi wa wanajihadi tangu mwaka 2015.

Kumekuwa na mapinduzi mawili ya kijeshi nchini Burkina Faso mwaka huu huku viongozi wa wote wawili wakiahidi kumaliza ghasia hizo.