Jumatano , 24th Feb , 2016

Hekari zaidi ya 545 za mahindi na mpunga zilizoko katika kijiji cha Nanjulu tarafa ya Mandawa wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi zimesombwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha ambapo kaya 231 zinaishi katika maisha magumu kwa kula matunda.

Wahanga hao wakiwemo viongozi wa taasisi ya utafiti na maendeleo naliendele wametembelea maeneo yalipo kuwa mashamba hao nakukuta mazao yamesombwa na maji ambapo mratibu mazao jamii ya mizizi kitaifa Daktari Geoffrey Mkamilo amesema imewalazimu kupeleka mbegu zinazozaa kwa muda mfupi ili wahanga hao wapate kujikwamua kimaisha baada ya miezi miwili ijayo kuanzia sasa.

Mtafiti wa kituo cha utafiti wa mazao jamii ya mizizi cha Naliendele ametoa sampuli ya muhogo kwa wananchi hao lakini akastaajabishwa na wananchi hao kugombania na kunyang'anyana kutokana na kukosa chakula kwa muda mrefu ambapo wamesema huishi kwa kula matunda ya porini.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi.Mariamu Mtima akipokea mbegu hizo ameshukuru kituo cha mbegu cha Naliendele kwa kutoa mbegu hizo ambazo zitawafanya wahanga hao kurudi katika hali ya kupata chakula kwa mda mfupi sambamba na kuwataka vijana waache kucheza bao badale yake walime iliwaondokane na njaa na umasikini.

Chanzo ITV