
Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza Aidan Eyakuze
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 26, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, kufutia utafiti uliofanywa na shirika hilo kuhusu uelewa wa wananchi juu ya makato ya tozo na shughuli za maendeleo zinazofanywa kupitia tozo hizo.
"Nadhani wananchi wako tayari kuchangia katika maendeleo iwe kwa kodi ama tozo wakielimishwa na wakielaelezwe kwamba tunafanya hii kwa matumizi haya, wajue bajeti hiyo inatumikaje na wao watanufaika vipi na jasho lao, tujue tupewe taarifa na tushirikishwe katika maamuzi kama hayo nadhani itasaidia sana," amesema Eyakuze