Jumatano , 11th Nov , 2015

Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Mjini kimeshauri wananchi na watumishi wa serikali kuacha kujadili masuala ya kisiasa badala yake wafanye kazi kwa bidi ili kuleta maendeleo.

Kaimu katibu wa CCM mkoani Iringa Bw. Elisha Mwampashi

Kaimu katibu wa CCM mkoani Iringa Bw. Elisha Mwampashi amesema, kila mtu awajibike kufanyakazi kwa juhudi ili kuleta mafanikio kwa taifa letu.

Bw. Mwampashi amesisitiza jamii kujihusisha na masuala ya kisiasa kwani kushindwa kutimiza wajibu wake ni jambo litakalopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya taifa kwa ujumla

Hata hivyo, Bw. Mwampashi amesema, ili nchi iwe na maendeleo chanya katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kielimu na kiutamaduni wanapaswa kuwepo kwa viongozi waadilifu.