Jumanne , 10th Feb , 2015

Wananchi wa manispaa ya Iringa wametakiwa kujitokeza katika zoezi la uandikishaji kwenye daftari la kupigia kura pindi zoezi hilo litakapotangazwa ili kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu.

Katibu mkuu baraza la wanawake taifa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHEDEMA, Bi. Grace Tendega

Katibu mkuu baraza la wanawake taifa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA GRACE TENDEGA ameyasema hayo katika mkutano wa baraza la wanawake wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA uliofanyika katika viwanja vya mwembetogwa.

Naye naibu katibu mkuu wa chama hicho KUNTI YUSUPH amewataka wanawake na wananchi kwa ujumla kutokujitokeza kuipigia kura katiba inayopendekezwa kwa kuwa haijazingatia matakwa ya watanzania.

Hata hivyo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama hicho CHIKU ABWAO amewataka wanawake wa chama hicho kufanya kazi kwa kujituma ya kuwaelimisha wanawake wenzao ili waweze kukisaidia chama kupata ushindi katika uchaguzi mkuu.