Naibu Waziri wa Ardhi, Ridhiwani Kikwete
Kikwete ameyasema hayo katika Kijiji cha Ngage wilayani Simanjiro mkoani Manyara wakati alipofika kusikiliza na kutatua mgogoro wa ardhi unaomkabili mbunge wa jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka na Nancy Yese ambaye ni mtoto wa rafiki wa mbunge huyo na kugundua kuna udanganyifu ndani yake.
"Nilichogundua hapa kuna udanganyifu maana mmesema Yese hakuwa na nyumba wakati tumeenda na tumeikuta, sasa nikuombeni sana kutaneni wenyewe malizaneni, kaeni kwenye meza zungumzeni na kama kuna jambo mnalihitaji katika ardhi hii mtaliweka wazi na kulitatua hasa ikizingatiwa nyinyi ni ndugu na marafki wa karibu maana sisi tukija ni kuamua kwa mujibu wa shseria," amesema Niabu Waziri Kikwete.
Naibu Waziri kikwete alifika katika eneo hilo ili kutatua mgogoro wa ardhi wa shamba la ekari 3,500 ambalo linadaiwa kumilikiwa na familia ya marehemu Mzee Yese ikiongozwa na binti yake Nancy Yese huku baadhi ya wakazi wakiongozwa na Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka wakidai Yese anamiliki sehemu tu ya shamba hilo isiyozidi ekari 500.
Awali baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na Mheshimiwa Ole Sendeka walikanusha madai ya watoto wa mzee Yese kwamba baba yao alijenga nyumba na kuishi katika eneo hilo ili kuthibitisha umiliki wa shamba hilo.
Kutokana na madai hayo Niab u Waziri Kikwete aliamua kuzuru kwa kutembea kwa miguu kwa zaidi ya saa 3 ndani ya shamba hilo ili kujionea kwa macho yake baadhi ya vithibitisho vya umiliki wa shamba hilo na kukagua makazi na nyumba iliyodaiwa ni ya Yese.
Katika hali ya kustaajabu yalikutwa mabaki ya nyumba ambayo imechorwa na kusainiwa na mzee Yese ambaye ni mmiliki wake tarehe 21/11/2001 jambo lililompelekea Mheshimiwa Kikwete kuamini kuna kuna udanganyifu katika mgogoro huo wa ardhi kwani baadhi ya wakazi hao walidai eneo hilo halina nyumba kitu ambacho hakikua na ukweli ndani yake.
Katika kumaliza mgogoro huo wa ardhi Naibu Waziri Kikwete aliwataka wakazi hao wakiongozwa na Mbunge wao kukaa pamoja na familia ya Yese kwa uwazi na ukweli na kama wanahitaji eneo hilo kwa ajili ya ufugaji, malisho au kilimo basi wakubaliane na familia hiyo badala ya kulumbana.



