Jumatano , 18th Mei , 2022

Mke na mume wakazi wa Mtaa wa Lwenge, Halmashauri ya Mji Geita, wamenusurika kifo baada ya kutuhumiwa kuiba nyanya kwenye shamba la mkulima wa Nyanya ambaye aliibiwa mazao yake jana na leo asubuhi Mei 18, 2022.

Mke na mume wanaotuhumiwa kwa wizi

Wakizungumza kwenye ofisi ya serikali za mtaa huo, watuhumiwa wa tukio hilo wamesema kuwa wao walikuwa wanapalilia shamba la Miwa wakashangaa kundi la watu limewavamia .

Kwa upande wao wamiliki wa shamba hilo wanasema njia waliyotumia kuhakikisha wanamkamata mtu aliyeiba mazao yao.

Mtendaji wa Kata ya Kalangalala Hamad Hussein, amekiri kutokea kwa tukio la kukamatwa wezi kwenye Kata hiyo huku akiwataka wananchi kujihusisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato ili kuepukana na shughuli za kujivunjia sheria za nchi.