Alhamisi , 21st Jul , 2016

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mara, wale wote watakaoendeleza uchochezi na migogoro katika eneo la Mgodi la kampuni ya ACACIA North Mara bila kujali kiongozi.

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.

Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni katika vijiji vya Matongo, Nyabichene, Mkoani Mara wilayani Tarime,wakati wa utoaji taarifa ya kamati aliyoiunda kufuatilia chanzo cha mgogoro yote ambayo imekua ikitokea baina ya wananchi na wawezaji wa mgodi huo.

Mhe Muhongo amesema hawezi kukubali kuona kila kukicha migogoro inaendelea kuibuliwa na kusababisha machafuko na shughuli za kiuchumi kukwama na kwamba hali hiyo imefikia mwisho.

Waziri huyo ameongeza kuwa kamati aliyoiunda iliwahoji wananchi 4,400 wanaozunguka eneo hilo kwenye vitongozi 80 kwa lengo la kumaliza migogoro hiyo hivyo mapendekezo aliyotolewa yatafanyiwa kazi na serikali.

Prof. Muhongo amesema kuwa masuala yaliyopendekezwa na kamati ikiwemo suala la ulipwaji wa fidia kwa wananchi yatafanyiwa kazi kwa muda uliopendekezwa na kwamba wananchi wanaostahili kulipwa watalipwa na wasio stahili hawatalipwa.