Alhamisi , 26th Jan , 2023

Kaimu Mkuu wa wilaya ya Nyanghwale mkoani Geita Fabian Sospeter ametangaza operesheni ya kuwasaka na kuwakamata watu wote wanaovamia hifadhi ya msitu wa serikali wa Miyenze  na kulima zao haramu la bangi

Amesema lengo la msako huo ni kuurudisha msitu huo uweze kutumika kwa ajili ya biashara ya miti na chanzo cha mapato wilyani humo

Kauli hiyo ameitoa kwenye baraza la rasimu ya makisio ya bajeti ya halmashauri 2023/2024 na kuwataka madiwani kwenda kuongea na wananchi ili waweze kuacha tabia hiyo mara moja kabla hawajanaswa na mkono wa sharia.

"Na kamati ya usalama inakwenda kuchunguza, kufatilia, kuona ni kina nani wapo ndani mule wanafanya kwa sababu kuna mifugo, kuna watu wengine wanalima bangi kwenye msitu wa serikali ni jambo la aibu"

"Kwahiyo kamati ya usalama inachukua jukumu kushirikiana na halmashauri kwenda kufatilia wamiliki wa mifugo waliopo ndani, wenye mashamba na wengine wote wanaofanya shughuli haramu ili kuweza kuchukua hatua", amesema Sospeter.

Kuhusu baadhi ya watumishi wasio waadilifu wanaokusanya mapato na kukaa nayo nyumbani kwa ajili ya matumizi yao binafsi mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani humo Saidi Madoshi anatoa maelekezo kwa kamati za fedha.

"Mkurugenzi kama tunaelewana vizuri hapo sisi chama tunaelekeza kila mwezi  hizi pos, mpewe taarifa ya kila pos kila mwezi ili mjue hizi fedha zipo salama vinginevyo kuna watu wanaokusanya ushuru huu mwenyekiti lakini kwa ajili ya watu fulani", alisema Madoshi.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John John ameahidi kwa kushirikiana na madiwani wenzie kutekeleza maagizo yote waliyopatiwa kutoka serikalini ili waweze kufikia lengo la kukusanya shilingi bilioni 31 kwa mwaka 2023/2024.

"Na niahidi tu mheshimiwa katibu tawala wetu na mkurugenzi na team ya mapato tutaenda kufanya vizuri, tutaenda kushirikiana vizuri  na tunaenda kushauriana vizuri na tutaenda kukusanya vizuri passport shida yeyote ", alisema John.

"Cause kila halmashauri inafanya kazi kwa bajeti na malengo yake kama mkusanyaji mapato atakaa na hela na serikali kwa maana kwamba ataathiri bajeti ya halmashauri ambayo kimsingi ndio inayopitishwa kwa ajili ya shughuli zinazoendelea kwa maendeleo ya wananchi na miradi ya wananchi kwa ujumla", alisema Mgema.

"Zile zinapochelewa kutufikia sisi kwenye kamati ya fedha kwa mfano na zinapochelewa kubenkiwa  maana yake zinachelewa kwenye kapu la halmashauri na zinapowahi kuingia kwenye kapu la halmashauri, maana yake sisi kama kamati ya fedha na kama baraza tunazipangia kwenda kwenye miradi mingine", alisema Yuda.