Jumatatu , 20th Oct , 2014

Baraza la Wanawake la Chama Chama Cha Demokrasia BAWACHA, jijini Mwanza nchini Tanzania wamewataka Wananchi waisome Katiba inayopendekezwa na kuielewa na ndio waweze kuipigia kura na sio kulazimishwa na maneno ya viongozi.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo taifa, BAWACHA Bi. Halima Mdee.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara jijini Mwanza Naibu Katibu wa Bawacha Taifa Kunti Yusuph amesema kuwa wananchi hasa wanawake wanapaswa kuelewa kipaumbele chao katika maisha yao ya kila siku.

Bi Kunti amewataka Wanawake kujua kuwa kipaumbele katika maendeleo yao ni kupata huduma bora za afya na kuepuka na mateso na manyanyaso yanayojitokeza na wala sio uwiano sawa wa asilimia hamsini kwa hamsini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa BAWACHA taifa Bi. Halima Mdee amesema kuwa kwa kuwa wanaamini ni rahisi kudanganyika kwa uwiano sawa katika Serikali lakini hilo halimsaidii mwanamke kuweza kupata mahitaji yake muhimu ikiwemo huduma izo za afya.