
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Kauli hiyo ameitoa hii leo jijini Dodoma, na kusema kwamba wanawake ni jeshi kubwa ambapo katika matokeo ya Sensa limedhihirisha ukubwa wanawake.
"Kati ya watu milioni 61.7, wanawake wapo milioni 31.6, sawa na asilimia 51, wanawake ni jeshi kubwa, na idadi ya wanaume wetu Tanzania, Simba wetu Tanzania ni milioni 30.053 sawa na asilimia 49 ya watu wote," amesema Rais Samia.
Kwa takwimu za Sensa zilizotolewa hii leo, Tanzania ina watu wapatao milioni 61.7