Jumapili , 22nd Aug , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameitaka Wizara ya Michezo kuhakikisha kuwa yanapoandaliwa matamasha ya michezo ya kila mwaka basi wanawake wanaocheza mpira wa miguu pia waangaliwe ili kuwajengea mazingira ya maisha yao ya baadaye.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo amitoa hii leo Agosti 22, 2021, wakati akipokea kombe la ushindi la Michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa Vijana wenye Umri chini ya Miaka 23 (CECAFA Challenge Cup 2021), na kusisitiza kwamba mifuko ya michezo iangalie hatma za wachezaji wanawake kwa siku za usoni.

Tazama video hapa chini