Waombwa kufungua maduka yaliofungwa

Monday , 17th Jul , 2017

Manispaa ya Kinondoni Dar es salaam imetoa siku saba kwa wafanyabiasha wenye maduka ambayo wameyafunga kwa sasa katika soko la Tegeta Nyuki kuhakikisha wanafungua maduka hayo ndani ya kipindi hicho vinginevyo watanyang'anywa na kupewa watu wengine.

Afisa Masoko wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Zahoro Hanuna ameiambia 'Kurasa' leo kwamba hatua ya wafanyabiashara hao kuyafungwa maduka hayo kunaikosesha serikali mapato huku kukiwa na idadi kubwa ya watu ambao wangependa kupangishwa na kulipa kodi.

Afisa masoko huyo amesema tayari walishatoa muda wa zaidi ya maizezi sita iliyopita lakini wamiliki hao walishindwa kufungua maduka hayo na kuwa muda wa siku saba ukipita hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa.