.jpg?itok=Otmp9W88×tamp=1473366450)
Shirika la Dawa Asili na Ulinzi wa Mazingira yake nchini Tanzania TRAMEPRO limetaka taratibu zilizotolewa na serikali tarehe kumi na tano Januari mwaka huu kupitia kwa waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu ziheshimiwe kwani lina lengo la kufanya maboresho ya kisheria katika huduma ya tiba asili.
Akiongea leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa TRAMEPRO bw. Boniventura Mwalongo amewataka wanachama pamoja na wote wanaohusika kutoa huduma za dawa asili nchini kuheshimu taratibu na sheria zilizopo wakati ambapo shirika hilo linaandaa semina za kuwaelimisha kuhusu dawa hizo na nia ya serikali kuhusu utoaji wa huduma hiyo..
Aidha Bw. Mwalongo amesema changamoto kubwa wanayopata ni kukosekana kwa tafiti nyingi pamoja na kukosekana na elimu ya kutosha kwa watendaji na watoa huduma wa tiba mbadala katika maeneo mbalimbali nchini.