
Octoba 13, 2022 zilisambaa video kwenye mitandao zikimuonesha mtahiniwa Iptisum Suleiman Slim akilalamikia kubadilishiwa namba ya mtihani wa darasa la saba, shule ya Chalinze Modern Islamic
Waziri wa elimu Prof. Mkenda amesema baada ya uchunguzi imebainika kuwa ni kweli mtahiniwa alibadilishiwa namba na kwamba watahiniwa wengine 7 walibadilishiwa namba za mtihani
"Baada ya video ile niliagiza mara moja uchunguzi ufanyike katika kituo hicho, na baada ya kufanya uchunguzi tumebaini na kujiridhisha kuwa ni kweli mtahiniwa alibadilishiwa namba ya mtihani, mitihani mitano aliyoifanya alitumia namba 40, lakini mtihani wa mwisho alibadilishiwa namba na kutumia namba 39"
"Baada ya kufuatilia zaidi, tulibaini watahiniwa wengine 7 walibadilishiwa namba zao za mitihani. Hivyo dosari hii ilitokana na uzembe kutoka kwa Msaidizi Mkuu wa Shule hiyo"- amesema Prof. Adolf Mkenda .
Aidha, kutokana na hali hiyo.... Waziri Mkenda amesema kwa mujibu wa sheria ya mitihani kifungu cha 4(8) kituo hicho kinafungiwa na kwamba wahusika waachishwe kazi