Jumanne , 12th Aug , 2014

Watoto wawili wa kijiji cha Rwerere kata Rwambaizi wilayani Karagwe Noviath Sarapion(14) na Kalen Dausoni ( 4) wamefariki dunia baada ya kunywa sumu ya kuoshea mifugo, wakidhani ni dawa ya kutibu kikoozi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera ACP Henry Mwaibambe

Watoto wawili wa kijiji cha Rwerere kata Rwambaizi wilayani Karagwe Noviath Sarapion(14) na Kalen Dausoni ( 4) wamefariki dunia baada ya kunywa sumu ya kuoshea mifugo, wakidhani ni dawa ya kutibu kikoozi.

Tukio hilo limetokea majira ya saa Nne asubuhi August 10 mwaka huu(Jumapili) katika kijiji hicho, huku mama yao akiwa ameenda kanisani kusali, na baba yao Sarapioni Gondo akiwa ameenda kusalimia majirani.

Mama yao aliyejulikana kwa jina la Mama Subi (35) ameeleza kuwa watoto hao ambao ni marehemu kwa sasa walikuwa wanasumbuliwa na kikoozi ambapo walichanganya chupa ya dawa ya mifugo badala ya dawa kikoozi iliyokuwa chumbani na kuinywa,wakiwa na dhumuni ya kutibu kikoozi walichokuwa nacho.

Katika harakati zakuokoa maisha ya watoto hao, mtoto mdogo Kaleni alifia katika Kituo cha afya cha Rwambazi kabla ya kupatiwa huduma, ambapo Noviathi aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la Saba shule ya msingi Rwele alifia njiani akikimbizwa katika hopitali ya wilaya Nyakahanga.

Kutokana na kuwepo tukio hilo la kuhuzunisha, jeshi la Polisi mkoani hapa,limewatahadharisha wananchi wote kuepuka kuchanganya dawa za matumizi tofauti katika makazi yao, huku likisisitiza umuhimu wa kuweka wazi matumizi ya dawa hizo kwa wanafamilia.

Kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa Henry Mwaibambe, akitoa maelezo juu ya vifo hivyo, amewataka wananchi kuondoa dhana ya usiri na kuelimisha jamii kwa kila jambo ili kuweza kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Wazazi wanapaswa kujitahidi kuendelea kuwaelimisha watoto kama kuna dawa imenunuliwa kwa malengo fulani kabla ya matumizi jitahidi kutoa maelezo kwa watoto na pia dawa ziwekwe mbali na watoto kama maelezo ya dawa yanavyoelezwa na dawa yoyote inaweza kuwa sumu ikiwa imetumika visivyo alisema Mwahibambe.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe, tayari miili ya marehemu imekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.