Watoto masikini katika moja ya nchi za Afrika
Shirika hilo la Overseas Development Institute (ODI) limesema mtoto mmoja kati ya watoto watano katika Kanda ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara au karibu milioni 148 watakuwa wanaishi kwa chini ya dola 1.90 kwa siku ifikapo mwaka 2030 muda wa mwisho uliowekwa na viongozi wa dunia kuondoa umaskini uliokithiri.
Kufikia 2030 ODI inakadiria kuwa asilimia 88 ya watoto wote wanaoishi kwa kiwango cha chini ya dola 1.90 kwa siku watakuwa katika Kanda ya Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwa imeongezeka kutoka asilimia 50 ya sasa.