Jumatano , 2nd Nov , 2022

Mkuu wa wilaya ya Magu Salum Kalli amewasimamisha kazi watumishi watano wa idara ya afya wasio waaminifu ambao wamekuwa wakitumia taaluma yao vibaya kwa kutoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa, kuomba rushwa pamoja na kuhusika na upotevu wa dawa katika Zahanati na vituo vya afya wilayani humo

Dc Kalli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi hao wa idara ya afya wilayani humo ambapo amesema kwa sasa wamebainika watumishi hao watano lakini ataendelea kufuatilia ili kubaini kama kuna wengine wachukuliwe hatua na ikiwezekana nafasi zao zichukuliwe na watumishi waadilifu

‘Kwanza rushwa haikubaliki lakini pili kutumia udanganyifu marufuku wapo watumishi ambao tumeshawabaini wapo zaidi ya watumishi watano lakini tayari tumeshaanza kuchukua hatua kwa yale ambayo wameanza kuyachukua kama wanafanya huduma lakini wamekuwa wakienda kinyume na maadili lengo ni kuhakikisha wanakuwa waadilifu tunamwakilisha Rais vizuri kazi hiyo nimeainza kwa kuwasimamisha kazi hao ambao wameonyesha utovu wa nidhamu’

Mkuu wa TAKUKURU wilayani Magu Neema Mzeru amesema hawatavumilia vitendo vya rushwa katika wilaya hiyo
"Lakini suala la kupokea rushwa ili kutoa huduma sisi TAKUKURU tunalipinga na yeyote yule atakayepokea rushwa ili kutoa huduma tutakapombaini tutamchukulia hatua tujitahidi kutoa huduam pasipo kudai chochote kile"