Jumatano , 2nd Sep , 2020

Baadhi waliokuwa wafanyakazi wa Hospitali ya Tumaini iliyokuwa Upanga Jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kuingilia kati hatima yao kufuatia kudai kuondolewa kazini bila ya kulipwa stahiki zao za msingi.

EATV  imekutana na kundi hilo la waliodai kuwa wafanyakazi wa ngazi ya uuguzi wakiwa katika maandamano ya pamoja wakitafuta taasisi inayoweza kuwapa msaada wa kisheria kwa kuwa hawana uwezo wa kufanya hivyo.

Awali wakielezea sakata zima wamesema yalikuwepo madai ya Hospitali kushindwa kujiendesha ndipo akapewa jukumu Erick Mramba kama mfilisi ili kusimamia uuzwaji wa mali zote na ulipwaji wa madeni pamoja na stahiki za watumishi ikiwemo mishahara na kuinua mgongo lakini malipo yao hao yamekuwa na msuguano na kukwama.

Kutokana na madai hayo yaliyoekekezwa kwa Mfilisi Erick Mramba EATV ikamtafuta kutoa maelezo yake kuhusiana na mchakato huo alivyoumsimamia pamoja na kutaka kujua ukweli kuhusiana na madai hayo ya wafanyakazi.