Vijana wa Kiteto
Mbele ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, George Katabazi, wananchi hao wamesema hawana matumaini tena kama watakuwa na vijana wa kuwasaidia baadaye kutokana na wengi wao kujihusisha na madawa ya kulevya.
"Bangi inauzwa hadharani ni makundi kwa makundi ya vijana wanavuta bangi kutwa, hatuna matumaini kesho kama kuna vijana wa kutusaidia, tuna mateja wa baadaye kinachoonekana," amesema mmoja wa wananchi
Akizungumzia madawa hayo Kamanda Katabazi amesema, wazazi, jamii na viongozi wa dini wanayo nafasi ya kubadili tabia za watoto wao kutenda matendo mema huku akisema Jeshi la Polisi nalo litaendelea kuwa mstari wa mbele kukabiliana na mapambano hayo.
"Mambo yote hayawezi kufanywa na polisi peke yake, jamii wazazi wanajambo la kufanya viongozi wa dini masheikh na wachungaji mnanafasi ya kutenda kubadilisha vijana hawa sisi tutawakamata na kuwapeleka mahakamani ila haitoshi," amesema RPC Katabazi








