Jumanne , 15th Jan , 2019

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki huenda ndiye waziri pekee ambaye amehudumu katika wizara nyingi kwenye kipindi cha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli.

Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Wakati akitangaza kwa mara ya kwanza baraza la Mawaziri lililokuwa na mawaziri 19 mwishoni mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe alimteua Angela Kairuki kuongoza Wizara ya Utumishi na Utawala bora.

Oktoba 2017, Angela Kairuki aliteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kushika nafasi ya Waziri wa Madini baada ya kuvunjwa kwa iliyokuwa Wizara ya Nishati ya Madini ambayo ilikuwa ikiongozwa na Sospeter Muhongo ambaye ni Mbunge wa Musoma Vijijini.

Januari 6, 2019 kwa mara ya tatu Rais John Pombe Magufuli alimteua Angela Kairuki kuwa Waziri mpya wa Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji, na kumfanya kuwa waziri pekee ambaye amehudumu wizara nyingi kwenye utawala wa Rais John Pombe Magufuli.

Hapo inaonesha katika kipindi cha miaka 3 Rais Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri mara 3. Mawawiri walioondolewa kwenye nafasi zao ni Nape Nnauye, Charles Kitwanga, Mwigulu Nchemba, Charles Tizeba, Jumanne Maghembe, pamoja na Gerson Lwenge.