
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Hasunga ameyasema hayo alipotembelea eneo la Ihumwa ambapo ujenzi wa ofisi mpya za Wizara ya Kilimo zimeanzwa, Jijini Dodoma ambapo amesema Mwl. Nyerere ndiye aliyetoa wazo la Dodoma kuwa makao ya Chama Tawala pamoja na serikali lakini kwa miaka kadhaa wazo hilo lilikuwa halijawahi kutekelezwa na kuongeza kuwa Rais Magufuli ndiye amelitekeleza kwa vitendo.
“Napenda nimpongeze Mhe. Rais wetu kwa kulisimamia wazo hili la kuwa na eneo maalum na rasmi la kuwa ofisi kwa Wizara zote na moja kati ya faida ni kuwa Wananchi ambao wamekuwa wakisafiri kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata huduma katika ofisi za umma, sasa watapata unafuu wa kuhudumiwa katika eneo moja kama hapa, ambapo kila Wizara itapatikana", amesema Waziri Hasunga.
Waziri Hasunga ameongeza kuwa, jambo hili ni sawa na utekelezaji wa Oparesheni sogeza ambapo, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alianzisha katika mwaka 1974 lengo likiwa ni kuhakikisha Wananchi wanakaa pamoja ili Serikali iwahudumie kwa haraka zaidi na kwa ufanisi zaidi.