Ijumaa , 2nd Aug , 2019

Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabia nchi yanayochangia kupungua kwa uzalishaji na tija ya mazao, uhaba wa malisho ya mifugo na rasilimali maji, teknolojia duni za kuhifadhi mazao baada ya mavuno na uhaba wa miundombinu ya masok

Changamoto hizo zimebainishwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akimkaribisha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika ufunguzi wa Sherehe za Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Waziri Hasunga amesema Wizara ya Kilimo imeandaa mkakati wa Taifa wa miaka 10 wa usimamizi wa Mazao baada ya Kuvunwa ili kukabiliana na baadhi ya changamoto hizo za upotevu wa mazao baada ya kuvuna.

Katika utafiti uliofanyika, inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 watu watakuwa bilioni tisa (9) na hivyo mahitaji ya chakula yatakuwa asilimia 60 zaidi ya mahitaji ya sasa, hivyo mkazo utakuwa kuzalisha chakula kati ya asilimia 50 – 70 zaidi ya sasa, udhibiti wa upotevu wa mazao ya chakula ni suala muhimu na la kipekee”, alikaririwa Mhe Hasunga.

Aidha Waziri Hasunga ametaja mkakati huo kuwa una malengo makuu tisa ambayo ni kujenga uelewa kuhusu usimamizi wa mazao baada ya kuvuna ili kuboresha ufanisi na kupunguza upotevu wa mazao katika mnyororo wa thamani.