
Kundi la ng'ombe
Hatua hiyo inachukuliwa ili kuondoa malalamiko ya wafugaji kutozwa tozo mbili tofauti pindi mifugo inapokamatwa imeingia katika hifadhi hiyo.
Akizungumza na na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, Dkt. Ndumbaro amesema amefikia uamuzi huo ili kuwapa nafasi wafugaji wataokamatwa wakiwa wameingiza mifugo yao kati ya Hifadhi hizo kuamua kulipa kiasi hicho cha pesa kwa Uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere au kwa Uongozi wa Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya ILUMA kwa vile kote faini ni sawa.
'' Kwa mamlaka niliyonayo kama Waziri mwenye dhamana natangaza kuanzia leo faini ni kiasi cha shilingi laki moja kwa kila kichwa cha ng'ombe'', amesema Dkt. Ndumbaro.