Jumanne , 18th Jan , 2022

Tume ya Ushindani nchini (FCC) imetakiwa kutoa sababu za kupanda kwa bei za vinywaji baridi ndani ya siku tatu.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ashantu Kijaji

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ashantu Kijaji kufuatia hali ya kuadimika na kupanda kwa bei ya vinywaji baridi ikiwemo soda.

Wakati huohuo, waziri Kijaji ametoa muda wa siku 7 kwa Tume ya Ushindani kutoa sababu za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi sambamba na kueleza hatua zilizochukuliwa na tume hiyo kukabiliana na hali ya kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.