Jumanne , 13th Aug , 2019

Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unatarajiwa kuanza kufanyika leo Jumanne ya Agosti 12,2019 ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi anatarajiwa kukabidhiwa

Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa ngazi za Mawaziri.

Waziri Kabudi amesema hayo wakati akifanya ukaguzi wa pikipiki mpya zitakazotumika katika mapokezi ya viongozi na wakuu wa nchi na Serikali wa SADC, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa SADC wa Dar es salaam.

Kwa niaba ya Serikali, Waziri Kabudi ameeleza kuridhishwa na kufurahishwa kwa namna vyombo vya habari nchini vinavyoripoti kizalendo mkutano huo wa SADC jambo ambalo limeongeza uelewa wa wananchi kuhusu SADC.

Katika tukio jingine Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Denmark Nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet.