Waziri Lukuvi ameyasema hayo kwenye ziara mkoani Mwanza alipotembelea Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya jiji la Mwanza na kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi hilo la ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi linakamilika kwa wakati.
Amewataka wakuu wa idara za ardhi nchini kusajili hati za viwanja kwa wanaohitaji ardhi kwa kutumia majina yanayotambulika kwenye vitambulisho vya taifa NIDA ili kuepuka udanganyifu ambapo kodi hiyo ipo kisheria.
Waziri Lukuvi pia amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanapima maeneo yote yakiwemo mamlaka za viwanja vya ndege, hifadhi za wanyama na misitu taasisi zinazomiliki ardhi na wizara zote kupimwa.





