Alhamisi , 15th Nov , 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuhakikisha zinachukua hatua kali dhidi ya watu wote watakaobainika wanaingiza nchini bidhaa za chakula na mafuta ya kupikia kwa njia za magendo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Kadhalika, Waziri Mkuu aziagiza mamlaka husika kuhakikisha zinaendelea kudhibiti uingizwaji holela wa bidhaa mbalimbali za vyakula visivyokuwa na virutubisho yakiwemo mafuta ya kupikia na kutoa adhabu kali kwa wafanyabiashara watakaobainika kuingiza bidhaa hizo nchini.

Mbunge huyo alihoji kuhusiana na suala la uagizwaji wa mafuta ya kupikia kutoka nje kama unazingatia sheria iliyopitishwa na Serikali ambayo inayolazimisha vyakula na mafuta ya kula kuwekwa virutubisho.

"Sheria hiyo pia inataka vyakula vyote vikiwemo vile vilivyoagizwa kutoka nje ya nchi na vinavyozalishwa hapa nchini yakiwemo mafuta ya kupikia, lazima viwekewe virutubisho. Wafanyabiashara wanapaswa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kulinda afya ya mlaji"

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Kiteto Zawadi Koshuma aliyetaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kukuza utalii nchini kupitia fukwe zilizopo katika ukanda wa bahari na maziwa, ambazo  zimeachwa bila kuendelezwa.