Ijumaa , 2nd Dec , 2022

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Mifugo ya Uvuvi nchini  kuweka juhudi za ziada kwenye uzalishaji wa punda nchini, katika kipindi hiki ambacho wanyama hao wapo hatarini kutoweka Afrika kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya nyama yake nchini China.

Punda

Akimwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kwenye kongamano la kujadili ustawi wa  punda Afrika, ambapo amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania inaendelea kusimamia katazo la uchinjaji wa punda nchini.

Aidha Wizara ya Mifugo imeagizwa kutenga bajeti ya kuendeleza uzalishaji wa punda pamoja na kutoa elimu zaidi kuhusu fursa za  ufugaji wa punda nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo amebainisha kuwa Senegal wataendelea kufanya tafiti zitakazo kuja na suluhisho la kuongeza uzalishaji wa Punda Afrika.