
Mamlaka za nchi hiyo zinatanabaisha kwamba takribani watu 6,500 ambao wameshtakiwa kwa makosa ya kumiliki kiasi kidogo cha bangi watanufaika na msamaha huo.
Mpaka sasa hakuna aliyefungwa gerezani kwa mashtaka hayo.Msamaha huo utawafanya washukiwa kupewa ajira, nyumba na fursa ya elimu . Wakati wa kampeni za Urais , Biden aliahidi kuondoa kesi za washukiwa wa bangi na kusamehe kesi zao.
Rais huyo kutoka chama cha Democratic amesema kwamba atawaeleza magavana wote kwenye majimbo nchini humo kuweka uratatibu wa kusamehe washukiwa wa bangi.
Amesema kwamba imefika mahali bangi inachukuliwa kama dawa hatari za kulevya aina ya heroin . Tayari bangi imehalalishwa katika majimbo 19 ikiwemo Washington DC. Matumizi ya matibabu ni halali katika majimbo 37 na maeneo matatu ya Marekani.