Alhamisi , 23rd Jul , 2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imebadilisha majina ya majimbo matatu, likiwemo jimbo la Chilonwa, ambalo kwa sasa linaitwa Chamwino, Jimbo la Mtera limebadilishwa na kuitwa Mvumi, na Jimbo la Kijitopele lililopo Wilaya ya Magharibi B linaitwa jimbo la Pangawe.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 23, 2020, na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, Jijini Dodoma, ambapo ameongeza kuwa mabadiliko ya majina kwa majimbo hayo hayahusishi ongezeko wala upungufu wa majimbo ya uchaguzi na yatabaki yale yale.

"Tume haijagawa majimbo, majimbo ya uchaguzi yanabaki kuwa 264, kama ilivyokuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015" amesema Jaji Mstaafu Kaijage.

Aidha Tume hiyo imetangaza kuwa fomu kwa ajili ya uteuzi wa wagombea wa Kiti cha Urais zitaanza kutolewa kuanzia Agosti 5 hadi 25, huku fomu za wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani zitaanza kutolewa Agosti 12 hadi 25, 2020.

Tazama video hapa chini.