
Kuelekea mkutano baina yao ndani ya siku chache zijazo kufuatia mazungumzo baina ya viongozi hao na rais wa Marekani, Donald Trump na wale kutoka umoja wa Ulaya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekosoa masharti yaliyowekwa na Urusi juu ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine akisema yanalenga kuidhoofisha Ukraine na kuonyesha kwamba hayuko tayari kumaliza vita.
"Mchezo wake wote ni kutudhoofisha iwezekanavyo," Volodymyr Zelensky alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari mtandaoni baada ya mazungumzo ya simu kati ya Vladimir Putin na Donald Trump hapo jana Jumatatu Agosti 18.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameunga mkono wazo la Trump kwa Ukraine na Urusi kuacha kushambulia miundombinu ya nishati kwa siku 30, lakini ameweka masharti ya kutekeleza hilo. Wakati wa mkutano wao wa kilele huko Alaska, kiongozi huyo wa Urusi alimwambia rais wa Marekani kuwa anataka mikoa ya mashariki ya Donetsk na Luhansk - na angeacha maeneo mengine ya Ukraine yanayoshikiliwa na wanajeshi wake huku pia akilihitaji eneo la Donbas.
Wakati wa mazungumzo ya simu kati ya Vladimir Putin na Donald Trump, Putin alisema kwamba yuko tayari kukutana na Volodymyr Zelensky katika mkutano ambao unaweza kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Agosti, 2025 kufuatia mazungumzo baina ya viongozi hao na viongozi wengine kutoka umoja wa Ulaya waliomtembelea Rais Trump ili kusitisha vita hivyo.