Jumapili , 5th Jul , 2015

Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe ametangaza majina ya watanzania 99 wanaodaiwa kuficha mabilioni ya fedha katika benki moja nchini Uswisi.

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo akiwa katika moja ya Mikutano ya kukitangaza chama na kuomba ridhaa ya Watanzania kukipokea.

Zitto Kabwe ametangaza majina hayo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na chama hicho katika viwanja vya Mwembeyanga Jijini Dar esa Salaam, ambapo amesema orodha hiyo ni kutoka benki tawi la benki moja ijulikanayo kama benki ya HBC,

Zitto ambaye hata hivyo hakuyataja majina hayo kwa kile alichodai kuwa ni kubwa na kisheria ameyakabidhi kwa vyombo vya habari ili kuhakikisha kila mtanzania anafahamishwa.

Zitto amesema kuwa kiasi cha karibia trilioni 1.3 katika benki mbalimbali za nje za watanzania ambapo serikali inatakiwa kutoa majibu ya fedha hizo zipi ni za watu halali na zipi ambazo zimefichwa na mafisadi.