Jumanne , 23rd Jun , 2020

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amekamatwa leo Juni 23, 2020, na Jeshi la Polisi wakati akiwa kwenye kikao cha ndani cha kupokea Madiwani 8 waliojiunga na chama hicho wakitokea chama cha Wananchi CUF katika Jimbo la Kilwa Kusini.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, na kulia ni Mbunge Mstaafu wa Kilwa Kusini Selemani Bungara (Bwege).

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kusema kuwa hajakamatwa peke yake bali na viongozi wengine wa chama ambao waliambatana kwa pamoja.

"Ndugu Zitto alikuwa Kilwa Kusini kwenye ziara ya kupokea madiwani 8 wa CUF, ambao wamejiunga na chama chetu na leo walikuwa wanakabidhiwa kadi, Polisi wamevamia na wameondoka naye pamoja na Mbunge Bwege na viongozi kadhaa wa Kitaifa, hivyo jumla ni 7, wapo kituo cha Polisi Kilwa tunaendelea kufuatilia sababu na kwanini jambo hilo limetokea" amesema Ado Shaibu.

Taarifa kamili inafuata.