Zitto Kabwe awekwa chini ya ulinzi

Jumanne , 11th Jun , 2019

Chama Cha ACT Wazalendo kimethibisha kuwa kiongozi  wake mkuu, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, ameshikiliwa na vyombo vya usalama huko Zanzibar.

Zitto Kabwe

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Uenezi wa chama hicho Ado Shaibu, imeeleza kuwa sbabu kubwa ya kushikiliwa ni haruhusiwi kusafiri kwenda nje ya Tanzania.

''ACT Wazalendo inawajulisha wanachama wake na Watanzania kuwa kiongozi wetu wa Chama ndugu Zitto Kabwe, ameshikiliwa na mamlaka za Serikali tangu saa nane mchana leo'', imeeleza taarifa hiyo.

Aidha Ado ameongeza kuwa kiongozi huyo ameshikiliwa na maofisa wa Uhamiaji Zanzibar kwa maelekezo kuwa haruhusiwi kusafiri kwenda nje  ya nchi ambapo kiongozi huo alikuwa akisafiri kwenda nchini Kenya.