Ijumaa , 18th Dec , 2020

Wahitimu wanaomaliza vyuo hapa nchini wametakiwa kuonesha uvumilivu na kukazania matarajio wanayoyataka katika maisha ili waweze kuinuka kiuchumi na maisha kwa ujumla.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas

Hayo yamebainishwa hii leo Desemba 18, 2020, na Dkt.Hassan, Abbas Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ambaye pia ni msemaji wa Serikali wakati wa mahafali ya 25 ya chuo cha Uhandishi wa Habari cha DSJ leo jijini Dares salaam;ambapo ameongeza kuwa ukiwa na tabia ya kususasusa katika maisha hauwezi kupiga hatua.

"Nakumbuka wakati nimeteuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, nilipofika kuripoti kazini nikaambiwa kwa sasa hakuna gari lako, mpaka tukutafutie,mimi nikajisemea wacha 'nikomae'nitapanda bajaji ama boda na kazi nitaifanya nilionesha uvumilivu na umeniinua", amesema Dkt. Abbas.

"Nimeitoa habari hii ili iwe funzo kwenu, popote mtakapopewa fursa lazima muwe na uvumilivu na kujiwekea malengo ambayo unaweza kuyatekeleza na kuonesha mafanikio.na neno siwezi lipeni kisogo kwa kuwa litakufanya usiweze milele", ameongeza Dkt. Abbas.

Aidha Dkt. Abbas amewataka wahitimu wote kuwa na nidhamu ya kazi na wasisahau kumtegemea Mungu kwa kuwa yeye ndiyo kila kitu.