Arejea nyumbani kwao baada ya miaka 46

Jumanne , 26th Jan , 2021

Mwanaume mmoja nchini Kenya aliyejulikana kwa jina la Francis Indek Arachabon, amerejea nyumbani kwao baada ya kutoweka kwa miaka 46, ambapo inadaiwa kuwa wakati anaondoka alikuwa na miaka 29 na aliaga kwamba anaenda kumtembelea mjomba yake mkazi wa Kimilili.

Francis Indek Arachabon, aliyeondoka nyumbani kwao mwaka 1975 na kurejea 2021

Arachabon amerejea nyumbani kwao katika kijiji cha Kolait, Teso Kaskazini, kaunti ya Busia, mnamo Januari 17, 2021, na kupokelewa na kaka yake mwenye umri wa miaka 71 Erneo Okadapao, ambaye alieleza kuwa baada ya kumtafuta kwa muda mrefu aliahidiwa na mchungaji wa kanisa moja kwamba ndugu yake atarejea.

Inadaiwa kuwa Arachabon, baada ya kwenda kumsamilia mjomba yake, baadaye alielekea katika eneo moja linaloitwa Soy kwa lengo la kutafuta ajira na ndiyo ulikuwa mwanzo wa yeye kupoteza mawasiliano na familia yake.

Akisimulia maisha yake ya huko alipokuwa Arachabon, amesema kuwa kwa miaka hiyo yote alianzisha familia na mwanamke aliyemtaa kwa jina la Susan Tabolei, na kupata watoto watatu na kudai kwamba familia yake hiyo ndiyo chanze cha yeye kutoreea nyumbani.

Aidha mbali na yeye kuanzisha familia hiyo, alidai kwamba alikuwa akifanya kazi ya kulima mashamba ya watu na kupata fedha za kuihudumia familia yake.

Chanzo: Tuko swahili