
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa ametoka bungeni na kwenda nyumbani kwake kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba Mh. Lissu kwa sasa amekimbizwa hospitali kwa ajili ya kupata huduma na sasa yupo chumba cha upasuaji.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Taifa naye amesema Lissu yupo hospitali ya General.
Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa ajili ya kufahamu taarifa zaidi.