AbduKiba afunguka kuachana na mkewe

Jumanne , 4th Dec , 2018

Staa wa Bongo Fleva AbduKiba amekanusha ndoa yake kuvunjika na yeye kutengana na mke wake mpaka kumrudisha kwao na kusema mke wake aliumwa na ilibidi arudi kwao ili kupata matunzo bora zaidi na wana familia.

AbduKiba akiwa na mkewe.

Abdu Kiba amefunguka kwenye eNewz ya EATV na kusema kwamba yeye na mke wake hawajawahi kugombana wala kupishana kauli kwa kuwa wao ni watu wazima na yupo na mke wake mpaka sasa.

"Mimi na mke wake hatujawahi kugombana wala kupishana kauli kwa kuwa wao ni watu wazima siwezi kumuacha kwa kuwa nampenda sana mke wangu", amesema AbdulKiba.

Katika hatua nyingine Abdukiba ameeleza kwanini Alikiba hajatokea akiimba katika video ya King Music 'TOTO' na kusema kuwa, "Yeye ametuonyesha njia ya kupita na nyimbo ya kwanza wakati tunaiachia alikuwa anatuonyesha njia na sasa tumeshaifaham njia hivyo ameamua kutuacha ili sisi tufanye wenyewe".

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii zilizagaa taarifa zikidai kuwa ndoa ya mwanamuziki huyo imevunjika, ikiwa ni baada ya kuonekana katika video fupi na mwanadada wakiimba kipande cha wimbo wao mpya wa 'TOTO'.