Jumamosi , 20th Dec , 2014

Super Nyamwela ambaye amekuwa ni mtu wa karibu wa marehemu Aisha Madinda kwa miaka mingi kisanaa amekanusha taarifa kuwa mnenguaji huyo amefariki kutokana na 'Uteja'.

Super Nyamwela

Kufuatia hisia ambazo zimeendelea kutanda mitaani kuhusiana na sababu ya kifo cha aliyekuwa mnenguaji mahiri wa muziki wa Dansi, Marehemu Aisha Madinda, kutoka katika kamati ya msiba Super Nyamwela ambaye amekuwa ni mtu wa karibu wa marehemu kwa miaka mingi kisanaa amesema kuwa swala hili halina ukweli wowote.

Nyamwela katika mahojiano maalum na eNewz amegusia pia suala la ripoti ya uchunguzi wa mwili wa marehemu ambao ulifanywa siku ya jana na kusema kuwa, hakuna kitu kinachohusiana na dawa za kulevya ambacho wataalam wamegundua kuhusiana na kifo cha marehemu.

Marehemu Aisha Madinda amezikwa huko Kigamboni katika makaburi ya Mikwambe siku ya jana, na eNewz tunaitakia roho ya marehemu mapumziko mahala pema peponi aamin.

Msikilize Nyamwela akieleza hapa;

Marehemu Aisha Madinda