Jumatatu , 18th Oct , 2021

Mtayarishaji wa muziki Hannington Bugingo ambaye anapika albamu mpya Super Mega Star kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone amedokeza kuwa mpango wa albamu uko pale pale na mpaka sasa wamekamilisha nyimbo 6 kati ya 10.

Picha ya Msanii Jose Chameleone

Albamu hiyo ‘I am Joseph’ inatajwa kuwa ni kielelezo cha mafanikio ya zaidi ya miaka kumi kwenye safari yake ya muziki na ilikuwa itoke siku ya Uhuru wa Uganda Oktoba 9 mwaka huu lakini haikuwezekana kutokana na kuto kamilika kwa baadhi ya ngoma (4) ambazo zinapatikana humo.